728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 12, 2015

    IMEFICHUKA:KILICHOMPONZA SALIM MBONDE USAJILI YANGA HIKI HAPA!!



    Matarajio ya beki wa kati wa Mtibwa Sugar,Salum Mbonde kutua Yanga yameyeyuka ghafla.
    Simba ndiyo ilikuwa timu ya kwanza
    kumuwania beki huyo tegemeo wa Mtibwa Sugar kabla ya Yanga kutupa ndoano zake.

    Yanga ilitaka kumsajili beki huyo kwa ajili ya kuimarisha safu ya ulinzi ya kati kabla ya kumnasa beki wa KMKM ya Zanzibar, Hajji Mwinyi kwa dau la shilingi milioni 15.

    Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo, beki huyo ameondolewa kwenye orodha ya wachezaji watakaosajiliwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara. Chanzo hicho kilisema beki huyo alianza mwenyewe kujiondoa kwenye usajili wa Yanga kutokana na kuleta mapozi wakati akihitajika.
    “Hivi sasa anaomba mwenyewe kusaini kuichezea Yanga wakati tayari jina lake limeondolewa kwenye usajili wa msimu ujao.

    “Awali, wakati tukimhitaji alikuwa akileta pozi kwa kutopokea simu na wakati mwingine alikuwa akizima kabisa kwa makusudi hivyo tumemuona ni kama mchezaji msumbufu,hata kama akija atatusumbua tu.

    “Hivi sasa anatusumbua kwa kutupigia simu akiomba asajiliwe kwa dau dogo la Sh milioni 20, tofauti na awali alipotaka kusajiliwa kwa milioni 30,” kilisema chanzo hicho.

    Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, kuzungumzia usajili wao alisema“Sisi bado tunaendelea na usajili kwa wale wachezaji tunaowataka pekee, ukiona mchezaji tumemtambulisha, basi ujue tumemsajili, ukiona kimya ujue hatusajili.”
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: IMEFICHUKA:KILICHOMPONZA SALIM MBONDE USAJILI YANGA HIKI HAPA!! Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top