Mane:Klabu bingwa ya Bundesliga klabu ya Bayern Munich imeripotiwa kuwa mstari wa mbele kutaka kumsajili winga wa klabu ya
Southampton na timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane.Bayern inamtaka Mane 23 ili azibe mapengo ya majeruhi Arjen Robben na Frank Ribery.
Jenkinson:Klabu ya West ham imeripotiwa kujiandaa kumsajili tena kwa mkopo mlinzi wa Arsenal Carl Jenkinson badala ya kumsajili bure mlinzi Glen Johnson aliyeko huru baada ya kumaliza mkataba katika klabu ya Liverpool.
Chicharito:Klabu ya Inter Milan ya Italia imeanza kumfukuzia kwa karibu mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez "Chicharito" kwa ajili ya kujiimarisha tayari kwa msimu mpya wa Seria A.Manchester United inataka €15m ili kumuachia mshambuliaji huyo hatari raia wa Mexico.
Ayew:Klabu ya Swansea City imekamilisha usajili wa nyota wa Ghana Andrei Ayew akitokea klabu ya Marseille kwa uhamisho huru baada ya kugomea mkataba mpya toka kwa miamba hiyo ya zamani ya Ufaransa.
Trippier:Klabu ya Tottenham imepiga hatua katika mbio za kumsajili mlinzi wa klabu ya Burnley Kieran Trippier 24 baada ya kuripotiwa kuwa tayari kutoa kitita cha €5 m ili kutengea kipengere cha mauzo ya nyota huyo mwenye soka la shoka.
Lukaku:Klabu ya Roma imeripotiwa kuanza kuisaka saini ya mshambuliaji wa klabu ya Everton Romelu Lukaku ili kuongeza nguvu katika safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na mkongwe Fransesco Totti.Everton itamuuza Lukaku ikiwa kitita cha €45m kitatengwa kwa ajili ya nyota huyo Mbelgiji.
Dzeko:Kutoka gazeti la Daily Mail habari zinasema kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini anajiandaa kumuuza mshambuliaji wa klabu hiyo Mbosnia Edin Dzeko baada ya kupoteza imani naye.Dzeko 29 ambaye ametwaa taji la Epl mara mbili ataruhusiwa kuondoka Etihad ikiwa klabu zinazomtaka zitatoa kitita cha £20m.Vilabu vya Arsenal,Liverpool na Tottenham vimeripotiwa kumtaka staa huyo mrefu.
0 comments:
Post a Comment