Habari na Paul Manjale
Austin:Kocha wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers ameripotiwa kuingia katika mbio za kuisaka saini ya mshambuliaji wa QPR Charlie Austin 25 mwenye thamani ya
£15m.Mbali ya Liverpool vilabu vingine vinavyomtaka nyota huyo aliyefanya makubwa msimu uliopita ni Newcastle United na Chelsea.(The Sun)
Bender:Kocha wa Arsenal,Arsene Wenger inasemekana bado anatamani kumnasa kiungo mahiri wa ulinzi wa klabu ya Bayern Leverkusen Mjerumani Lars Bender mwenye thamani ya £18m ili kuimarisha safu yake ya kiungo cha ulinzi.(The Sun)
Falcao:Uhamisho wa mshambuliaji Radamel Falcao toka klabu ya Monaco kwenda Chelsea umekamilika jana jumamosi kilichobaki na uchunguzi wa afya wa nyota huyo ambaye kwa sasa yuko Chile akiwa na kikosi cha Colombia katika michuano ya Copa America.(Record)
Iker Casillas:Klabu ya Real Madrid imeripotiwa kuwa tayari kumuuza mlinda mlango wake No.1 Iker Casillas kwenda Tottenham kuchukua nafasi ya Hugo Lloris anayewindwa kuchukua nafasi ya David De Gea katika klabu ya Manchester United ambaye anasakwa kwa udi na uvumba na miamba hiyo ya Hispania.(Daily Mail)
Di Maria:Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Manchester City,Txiki Begiristain ameripotiwa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Angel Di Maria ili kuangalia uwezekano wa nyota huyo kutua Etihad.(The Sunday times)
Rooney:Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney ameripotiwa kuunga mkono kwa 100% mpango wa kocha wa klabu hiyo Louis Van Gaal kutaka kutumia kitita cha £40m kumsajili mshambuliaji nyota Harry Kane wa klabu ya Tottenham.Rooney anaamini Kane ana sifa zitakazomfanya afanikiwe Manchester United.(The Sun)
Deulofeu:Klabu ya Everton imefanikiwa imeshinda mbio za kumsajili mshambuliaji kinda wa Barcelona,Gerard Deulofeu kwa ada ya £3m.(Daily Mail)
0 comments:
Post a Comment