Habari na Paul Manjale
Umtiti:Vilabu vya Manchester City, Arsenal, Real Madrid and
Inter Milan vimeripotiwa kuanza kuigombea saini ya mlinzi kinda wa Lyon Samweli Umtiti 21.Umtiti nyota wa kikosi cha U-21 cha Ufaransa mwenye kudumu vyema nafasi ya ulinzi wa kati na kushoto anadhaniwa kuwa na thamani ya £11m.
Vidal:Klabu ya Barcelona imeripotiwa kufanikiwa kuipata saini ya mlinzi wa kulia wa klabu ya Sevilla Aleix Vidal kwa kitita cha €10m.Hata hiyo nyota huyo atasubiri mpaka hapo januari mwakani ndipo aanze kuitumikia klabu hiyo kutokana na kutumikia adhabu ya kufanya udanganyifu kwenye usajili.
Trippier:Klabu ya Liverpool imeingia katika mbio za kumsajili mlinzi wa klabu ya Burnley Kieran Trippier baada ya kuona hali ni ngumu kumpata mlinzi wa Southampton Nathaniel Clyne.
Meireles:Klabu ya Everton inajipanga kumsajili kiungo wa zamani wa klabu ya Liverpool Raul Meireles ambaye kwa sasa yuko katika klabu ya Fenerbahce ya Uturuki hii ni baada ya klabu hiyo kutangaza kumuuza nyota huyo katika kipindi hiki cha usajili.
Mirallas:Klabu ya Monaco imeripotiwa kuanza kuipigia hesabu saini ya winga wa Everton Kevin Mirallas kwa ajili ya kuongeza makali katika safu yake ya kiungo/ushambuliaji.
0 comments:
Post a Comment