Timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inaondoka usiku huu kwa usafiri wa ndege kwenda Cairo, Misri ambapo itaunganisha moja kwa moja kwenda mji wa Alexandria nchini humo.
Stars watachuana na Misri Jumapili mjini Alexandria katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Africa AFCON 2017.
“Timu inaondoka hapa Addis Ababa Ethiopia saa nne usiku kwenda Cairo Misri ambapo inatarajia kufika saa nane kasoro. Tukifika Cairo timu itaondoka moja kwa moja kwenda Alexandria kwa usafiri wa basi kwa takribani saa mbili, itafika alfajiri na kumpumzika.
Baada ya hapo tutaangalia ratiba ya mwalimu na Jumapili ndio mechi yenyewe”.Amesema Afisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto aliyeambatana na timu.
“Kocha (Mart Nooij) anashukuru kambi imekuwa nzuri, wachezaji wako fiti na wamefanya mazoezi katika ukanda wa juu,hivyo wanatarajia kufanya vizuri kwasababu wameonekana kushika mafunzo vizuri katika kambi ya wiki moja hapa Ethiopia”.
0 comments:
Post a Comment