SIMBA imefanya uamuzi mgumu kwa kumrudia kocha wake, Mserbia
Goran Kopunovic na huenda akatua nchini muda wowote kuanzia sasa kuendelea na kibarua chake.
Kocha huyo aliithibitishia Mwanaspoti jana Jumatano kwamba amezungumza na Simba juzi na jana jioni walikuwa kwenye makubaliano ya mwisho ambayo yalikuwa na asilimia kubwa ya kukamilika.
Habari za ndani zinasema kwamba Simba imempa Kopunovic ofa ya mshahara kiasi cha dola 6,500 sawa na Sh14 milioni kwa mwezi na pesa ya usajili dola 15,000 ambazo ni sawa na Sh32 milioni ili arudi kuifundisha klabu hiyo.
Kopunovic ameikubali ofa ya mshahara, lakini utata ukawa kwenye pesa ya usajili baada ya kutaka apewe dola 25,000 ambazo ni sawa na Sh53 milioni kwa makubaliano ya mkataba wa mwaka mmoja.
Chanzo ndani ya Simba kilisema baada ya kutofautiana, Simba walimwahidi Kopunovic atapewa jibu jana Jumatano baada ya uongozi wa klabu kukubaliana.
0 comments:
Post a Comment