728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 09, 2015

    RAMADHANI SINGANO ''MESSI' AIBWAGA SIMBA SAKATA LA MKATABA



    Hatimaye Ramadhan Singano ‘Messi’ ameibwaga klabu yake ya Simba na kutangazwa kuwa mchezaji huru katika kikao
    kilichofanyika leo makao makuu ya shirikisho la Soka Tanzania, TFF, maeneo ya Karume, Ilala, Dar es salaam.
    Katika kikao hicho, Simba iliwakilishwa na mjumbe wa kamati ya Utendaji na mwenyekiti wa kamati ya ufundi, Collins Frisch, wakati upande wa Singano alikuwepo Singano mwenyewe na mwenyekiti wa Chama cha wachezaji Tanzania,  SPUTANZA, Musa Kisoky huku  TFF ikiwakilishwa na katibu mkuu wake, Selestine Mwesigwa na msimamizi wa sheria na wanachama wa TFF, Eliud Mvela.
    Baada ya majadiliano ya pande zote mbili, huku kila mtu akitoa vielelezo vyake, kikao hicho kimeamua kwamba mikataba yote miwili imefutwa baada ya kuipitia, hivyo Singano na Simba waanze mazungumzo mapya.

    KWANINI MIKATABA YOTE IMEFUTWA, UPI NI SAHIHI?
    Hoja ya Msingi ni nani alichakachua Mkataba?
                             
    Imebainika kuwa mkataba wa Singano aliosaini Mei 1, 2013 na unaotakiwa kumalizika Julai 1, 2015 ndio sahihi, wakati ule wa Simba unaoonesha ulisainiwa Mei 1, 2013 na unatakiwa kumalizika Julai 1, 2016 sio sahihi.
    Kwa tafsiri rahisi, Simba ndio waliochakachua mkataba, lakini kutokana na busara za TFF ambazo tunazishuhudia mara nyingi wameamua kuwalinda Wakongwe hao wa soka la Tanzania.
    Kwanini wasema mikataba yote haipo wakati kwenye mfumo wa TFF mikataba yote ya wachezaji ipo?
    Simba wamelindwa na TFF, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba mkataba wa Singano ndio sahihi, hivyo kisheria ni mchezaji huru baada ya kushinda vita iliyogubikwa na kejeli na vitisho kutoka upande wa pili.
                                                                                                     
    AKISHINDWA KUMALIZANA NA SIMBA KATIKA MAZUNGUMZO MPYA ITAKUWAJE?

    Kama TFF wamewataka Singano na Simba kuzungumza upya kwasababu mikataba yote imefutwa, maana yake wakishindwana, Singano anachukua hamsini zake na sio lazima akubali kuendelea kuichezea Simba.
    Wakati huo huo, mtandao huu umefahamishwa kuwa, Katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa amemuandikia barua Singano ambayo nakala yake amechukua mwenyekiti wa SPUTANZA, Bwana Kisoky  ikithibitisha maamuzi yaliyochukuliwa  na kuwa ushidi wa maazimio ya kikao hicho.
    Ukweli ni kwamba TFF wamemaliza kiaina ili wasiwaumbue Simba waliokosea mkataba wao na wamewataka kufanya mazungumzo upya wakati ilitakiwa watangazwe kuchakachua mkataba.
    Simba wanajua fika kwamba mkataba wa miaka miwili wa Singano ndio sahihi ndio maana wamekubali yaishe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RAMADHANI SINGANO ''MESSI' AIBWAGA SIMBA SAKATA LA MKATABA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top