Barcelona,Hispania.
Mlinzi Dani Alves amekubali kuongeza mkataba wa
kuendelea kukipiga katika klabu yake ya Barcelona kwa miaka miwili zaidi.
Alves 31 aliyekuwa akiwindwa na vilabu vya Ac Milan pamoja na Manchester United alikuwa amebakisha wiki tatu pekee kufikia tamati ya mkataba wake wa sasa.
Kufuatia mkataba huo mpya Alves atakuwa Barcelona mpaka mwaka 2017 huku kukiwa na uwezekano wa kuongeza mwaka mmoja zaidi.
0 comments:
Post a Comment