Mchambuzi:Nicasius Coutinho Suso.
BARCELONA
Hakuna siri kuwa utatu wao mtakatifu ni hatari zaidi kwa Sasa duniani na ambao unakuwa unajiuliza kama unamkosa Chiellini pale Juventus khali itakuwaje. Hii ndio silaha kubwa kwa sasa kwao, hawahitaji kiungo mbunifu sana, wanahitaji mtu anayeweza kupiga pasi sahihi tu kuelekea miguuni kwa Suarez, Messi na Neymar. Hakuna wakati mgumu kukutana na Barcelona kama wakati huu.
JUVENTUS
Hawa wanafurahisha kutokana na namna ambavyo wameuvaa vizuri uhalisia wa jina UNDERDOG. kiuhalisia ni underdog sio kutokana na ubora wa kikosi Chao Bali ni kutokana na imani zetu mashabiki hasa tukitizama ligi wanayotoka ilivyo na suala zima la kushindwa kwao kufuzu hatua nzuri michuano iliyopita. Lakini kiuhalisia Juventus sio underdogs katika uhalisia wa soka. Hebu jiulize ni klabu ipi duniani Ina muunganiko bora wa sehemu ya kiungo kuliko Ile ya PIRLO, VIDAL, MARCHISIO, na POGBA. Jibu ni hakuna. Ndio maana tangu Robo fainali nilisema hawa watatembea vyema na Underdog syndrome na tutastuka siku tukimkuta kobe juu ya mti. Na hawajaniangusha katika hilo.
TUTEGEMEE NINI.
Juventus pasipo kupepesa macho watamkosa Chiellini kwa kiasi kikubwa, nilifurahishwa na walivyocheza na Madrid mechi ya kwanza lakini sikuwa muumini wa walichokifanya Santiago Bernabeu. Madrid walitoka sio kwa sababu ya ubora wa Juventus bali kutokana na ubutu wao siku Ile, hivyo huwezi kucheza na Barcelona vile ukategemea uwe salama. Ukicheza na Barcelona unatakiwa kuzuia Ile nia ya wale viungo kupeleka mipira mbele, walazimishe kucheza square passes (pass za pembeni) na sio pasi za mbele. Silaha hii Juventus wanayo, wanaweza kufanya hivyo kama Pep alivyofanikiwa dakika 75 za mwanzo pale Camp Nou kabla hajaamua kuranduka kichwa mwenyewe.
Upande wa pili Barcelona, hakuna la kutegemea zaidi ya Suarez, Neymar na Messi. Lakini Kuna kitu kimoja ambacho wengi hawakitizami kinaitwa Neymar. Pamoja na goli 10 za Messi lakini Barcelona wanahitaji ubora zaidi wa huyu mtu maana ndiye anayepata clear chances (nafasi za wazi) zaidi kuliko wengine wawili. Anatakiwa awe na umaliziaji bora kabisa na bahati amekuwa nayo katika Uefa champions League. Siku zote unapojitahidi kuwabana wale watatu Neymar huwa ndo anayesahaulika kwa kiasi kikubwa, hivyo kwangu Ana nafasi kubwa sana ya kuamua matokeo.
UAMUZI WA MSHINDI.
Kuna namna mbili za msingi ambazo Juventus wanaweza kuitumia. Kuzuia mirija ya mipira kwenda mbele lugha ya kiingereza Contain the Opponent Midfield. Wala wasiwaze kushambulia sana, hii itawadhoofisha Barcelona kiakili, kwa sababu tunawategemea kushambulia, hivyo watataka kuongeza kushambulia kutokana na kukereka na namna ya uzuiaji hiyo, ukiweza kuwazuia kwenye kiungo jambo ambalo Juventus wanaweza, unatumia breaks, counter attacks ambazo kwa kiasi kikubwa Juventus ni bora sana na Barcelona mi dhaifu sana. Hii ndio sehemu ambayo unaweza kuwafunga Barcelona kirahisi.
Njia nyingine kwa Juventus ni silaha ya wapigaji waliyonayo. Viungo wao wote wanaweza sana kupiga mashuti, na Barcelona ni moja ya timu ambazo sio za kichoyo katika hilo. Watakupa tu nafasi kutokana na aina hiyo, ukiwa na Tevez, Vidal, Marchisio na Pirlo ili ni moja ya maeneo ambayo unaweza kupata zawadi ya goli kwa urahisi kutoka kwa Barcelona.
Huku kwingine jambo la kwanza narudia tena, Neymar aweze kuwa mchezoni tu. Pamoja na ubora usiopingika wa Messi na kazi ya Luis Suarez lakini Neymar anabakia kuwa mchezaji asiyechungwa zaidi kati yao. Kwangu mimi huyu ndo kaibeba dhamana yao. Ninahisi nafasi alizopata Bale pale Bernabeu atazipata pia Neymar leo pale Berlin.
Daniel Alves + Rakitic. Hii ndio nguvu ya ziada ambayo naiona itawapa shida Juventus au kuleta nyongeza. Wakiweza kusogea vyema mbele na kuongeza kasi basi mechi inaweza kumalizika mapema.
ANGALIZO
Kutokuwepo kwa Chiellini kunaweza kuwa chachu ya kuiboresha Juventus tofauti na wengi wanavyofikiria, Hii ni kutokana na nidhamu anayokuwepo nayo mchezaji anayechukua nafasi na namna timu nzima inavyojaribu kumlinda.
Hakuna kitu kizuri kama kushambulia upande wa jirani ambako kiuhalisia hakutakuwa kumewekewa umakini zaidi, hivyo badala ya kutegemea madhaifu kwa aidha Bazzargli au Ogbonna ambao wanaweza kuziba nafasi sehemu nzuri ya kutumia ni kwa Bonucci.
MATOKEO.
Ninapata hisia Juventus watakuwa wa kwanza kupata goli.
Barcelona watatengeneza nafasi nyingi ambazo itawabidi kuzitumia. Wakiweza kupata walau goli moja mapema utakuwa rahisi zaidi kuwafungua Juventus.
Juventus Wakiweza kufika dakika 75 hawajafungwa Wana nafasi ya kushinda.
Barcelona wakipata goli mapema Kuna uwezekano tukashuhudia fainali yenye magoli mengi sana.
Nicasius Magic Pick (uchaguzi wangu wa maajabu).
1. Juventus nawachagua Lichtensteiner na Morata kama wachezaji ambao hawazungumzwi lakini watakaoleta balaa au wanaoweza kuamua mchezo.
2. Barcelona nawachagua Suarez na Dan Alves kama wachezaji wenye hirizi ya Barcelona leo.
Dakika 120 ni ngumu kama Barcelona atapata goli la mapema, lakini zikifika nahisi Juventus anaweza kuwa mshindi.
Hizi ndizo siku unazosubiri Individual Brilliance (uwezo binafsi) kwa Barcelona vs Team Work ya Juventus vionyeshe nani anaweza kumkalia mwingine.
Ahsanteni. By Nicasius Coutinho Suso.
Waweza toa maoni yako pia
0 comments:
Post a Comment