Tetesi na Paul Manjale
Pogba:Klabu ya Aston Villa imepata matumaini mapya ya kumsajili nyota wa Guinea na klabu ya Saint -Etienne Florentin Pogba baada ya kukataa mkataba mpya wa kusalia kwa mabingwa hao wa zamani wa Ufaransa.Florentin ni kaka wa kiungo Paul Pogba.
Vidal:Mkurugenzi wa klabu ya Juventus Guiseppe Moratta amesema klabu yake haina mpango wa kumuuza kiungo wake Arturo Vidal kwa kuwa kufanya hivyo itakuwa ni kosa kubwa sana kuwahi kufanywa na Juventus.Kauli hiyo ya Marrotta anazima uvumi kuwa Vidal ameshamalizana na klabu ya Arsenal.
Campbell:Klabu ya Real Sociedad ya Hispania imeripotiwa kuongeza kasi katika mbio za kutaka kumsajili nyota wa klabu ya Arsenal Joel Campbell.Campbell ambaye timu yake ya taifa ya Costa Rica inavaana na Hispania wiki hii katika mchezo wa kirafiki katika jiji la Leon anadhaniwa kuwa na thamani kati ya £5-10m.
Alderweireld:Klabu ya Chelsea imeripotiwa kuwa katika mazungumzo mazito na klabu ya Atletico Madrid kwa ajili ya kumsajili mlinzi Toby Alderweireld aliye kwa mkopo katika klabu ya Southampton.Nyota huyo ana thamani ya £14m
Cleverley:Kiungo wa klabu ya Manchester United Tom Cleverley 25 amekubali kujiunga na klabu ya Everton kwa mkataba wa miaka mitano baada ya mkataba wake wa sasa Old Trafford kufikia kikomo hapo Julai 1 mwaka huu.
Van Persie:Klabu ya Lazio baada ya kukata tiketi ya kucheza michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao imeripotiwa kuanza kusaka wakali ili kufanya vizuri katika michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.Habari kutoka vyombo mbalimbali zinasema Lazio imeanza kumnyemelea mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Robin Van Persie 31 na katika kutimiza leo hilo miamba hiyo ya Olimpico iko tayari kutoa kitita cha £10m.
0 comments:
Post a Comment