Habari na Paul Manjale
Kiungo wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil ameeleza jinsi anavyochukizwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo ya Ulaya.
Ozil ambaye mapema wiki hii amefanya mahojiano na gazeti la Bild la nchini humo amesema wazi wazi kuwa ana kerwa na tabia ya vyombo vya habari vya Ujerumani kumuuita Mjerumani- Mturuki.
Ozil ambaye ana asili ya Uturuki amesema ™Nadhani watu wamesahau kuwa nimezaliwa Gelsenkirchen (Ujerumani) na kukulia Ujerumani.
Najivunia kujua mengi kuhusu mambo mengi ya nchi hii kama nidhamu na mafunzo ya soka pia nimejifunza mengi kuhusu soka la Uturuki kupitia Television.
Ozil ameongeza ™Napenda watu wanione kuwa mimi ni mjerumani kama walivyo wajerumani wengine.Kwanini hawamuiti Sami Khedira Tunisian-German au Lukas Podolski na Miroslav Klose “German-Pols."?Alihoji Ozil.
0 comments:
Post a Comment