728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 07, 2015

    BARCA YATWAA UCHAMPIONI WA ULAYA,REKODI KIBAO ZAWEKWA

    Habari na Paul Manjale

    MCHEZO NA MATOKEO YAKE

    Klabu ya Fc Barcelona imeibamiza klabu ya Juventus magoli 3-1 katika mchezo mkali wa fainali wa ligi ya mabingwa Ulaya uliopita jana jumamosi katika dimba la Olympic mjini Berlin,Ujerumani.

    Barcelona ilipata bao lake la kuongoza dakika ya 4 ya mchezo kupitia kwa kiungo wake Ivan Rakitic kabla ya Juventus kusawazisha dakika ya 55 kupitia kwa kinda Alvaro Moratta.

    Louis Suarez alitumia vizuri makosa ya mlinda mlango wa Juventus Buffon na kufunga bao la pili dakika ya 68 kabla ya Neymar kufunga la tatu dakika ya 97.

    Kufuatia ushindi huo Barcelona inafikisha jumla ya vikombe vitano vya Ulaya huku ikiwa imetumia miaka 10 pekee kutwaa mataji manne ya michuano hiyo mikubwa na yenye utajiri wa kutupwa baada ya kufanya hivyo mwaka 2006,2008,2011 na 2015.

    Kufuatia ushindi huo Barcelona inaungana na vilabu vya Celtic 1966-67,Ajax, 1971-72,PSV 1987-88,Manchester United, 1998-99,Inter Milan, 2009-10,Bayern Munich, 2012-13,kutwaa mataji matatu makubwa ndani ya msimu mmoja.

    REKODI YAWEKWA

    -Barcelona yaweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza Ulaya kutwaa mataji matatu (treble) mara mbili

    -Juventus yafikisha fainali sita za Ulaya bila ya taji huku nahodha wa Barcelona Xavi akifikisha jumla ya michezo 151 ya ligi ya mabingwa Ulaya.

    -Ivan Rakitic aweka rekodi ya kufunga goli la mapema zaidi katika mchezo wa fainali baada ya kufunga dakika ya nne tu akiunganisha pasi safi ya kiungo Andres Iniesta aliyeibuka nyota wa mchezo huo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BARCA YATWAA UCHAMPIONI WA ULAYA,REKODI KIBAO ZAWEKWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top