BCC Swahili wameripoti kwamba, shirikisho la soka nchini Uingereza FA limesema kuwa halina haja ya kuandaa kombe la dunia la mwaka 2018 ama lile la mwaka 2022 nchini Qatar iwapo mataifa yanayoandaa yatapokonywa fursa hiyo.
Maafisa wa mashtaka wa Uswizi wanachunguza zabuni za michuano hiyo,ijapokuwa FIFA inasema kuwa hakutakuwa na ushindani mwengine wa kutolewa kwa zabuni hizo.
Katibu wa utamaduni nchini Uingereza John Whittingdale anasema kuwa Uingereza huenda ikachukua maandalizi ya kombe hilo iwapo itaombwa kufanya hivyo.
Lakini afisa mkuu wa shirikisho la FA Martin Glenn amesema kuwa Uingereza haina haja.
Akizungumza na SkyNews,Glenn ameongezea kwamba michuano hiyo ya mwaka 2018 itaandaliwa na Urusi kwa njia nzuri.
0 comments:
Post a Comment