728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 06, 2015

    COUTINHO ANOGEWA BONGO,AITAKA JEZI YA STARS

    Klabu ya St George ya Ethiopia, imetuma ombi la kumtaka Andrey Coutinho wa Yanga wakati kiungo huyo mshambuliaji raia wa Brazil akipiga hesabu za kupewa uraia wa Tanzania ili aichezee Taifa Stars.

    St George ambayo ni timu ya zamani ya Kocha wa Rwanda, Milutin Sredojevic ‘Micho’ imetenga dola 70,000 ili imsajili Coutinho ili ifanye vizuri katika ligi kuu ya nchi hiyo.

    Mmoja wa mabosi wa Yanga amesema, St George imetuma ombi la kumhitaji Coutinho na sasa viongozi wanamsubiri mchezaji huyo na Kocha Hans van Der Pluijm ili kufikia muafaka.

    “Kuna uwezekano mkubwa Coutinho akaondoka Yanga kwani St George imetoa ofa ya dola 70,000, hata hivyo tumeshindwa kutoa uamuzi hadi mchezaji atakaporudi na kocha pia,” kilisema chanzo chetu.

    Wakati huohuo, habari zinasema Coutinho ameuandikia barua
    uongozi wa Yanga akiomba
    asaidiwe kupata uraia wa
    Tanzania ili aichezee Taifa Stars kwani hana nafasi ya kuichezea
    Brazil.

    “Inaonekana amefurahia maisha ya Tanzania,kwani ametuomba
    ikiwezekana tumsaidie kupata uraia wa Tanzania ili aweze kucheza Taifa Stars,” kilisema chanzo hicho.

    Hata hivyo, alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Yanga, Jerry Muro alisema: “Sisi wenyewe tunasikia tu taarifa hizo, hazijafika kwetu.”

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: COUTINHO ANOGEWA BONGO,AITAKA JEZI YA STARS Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top