728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 06, 2015

    MAPEMAA!!HAZARD AMCHONGEA BENTEKE CHELSEA

    Habari na Paul Manjale

    Winga Eden Hazard ameitaka klabu yake ya Chelsea ifanye kila iwezalo ili iweze kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa Christian Benteke katika dirisha hili la usajili barani Ulaya.

    Akiwa nchini kwao Ubelgiji Hazard amevibia vyombo vya habari vya nchini kwao kuwa baada ya Didier Drogba kuondoka Chelsea basi mbadala wake siyo mwingine bali ni Christian Benteke.

    Hazard amesema " Nitakuwa ni mtu mwenye furaha sana pengine kuliko yeyote yule katika dunia ikiwa tu Christian atatua hapa.

    "Christian ni mchezaji mzuri sana tuna mahusiano mazuri mno timu ya taifa.Kama kuna kitu kitakacho nifurahisha basi ni kuona Christian akicheza Chelsea.

    Hazard ameongeza "Sisemi hivi kwa kuiona Aston Villa ni klabu ndogo la hasha bali ni kuwa Christian amefanya makubwa akiwa na klabu hiyo hivyo nadhani muda huu ni sahihi kwake kucheza ligi ya mabingwa.

    Benteke ameifungia Aston Villa magoli 12 katika michezo 13 ya ligi ya EPL tangu apone majeraha yaliyo mweka nje karibu mwaka mzima.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAPEMAA!!HAZARD AMCHONGEA BENTEKE CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top