728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, July 11, 2015

    RASMI BAYERN MUNICH YAMUUZA SCHWEINSTEIGER KWENDA MANCHESTER UNITED

    Wakati mwenyekiti wa Fenerbahce Aziz Yildirim akitangaza kuwa klabu yake imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Mdachi Robin Van Persie,31 kwa ada ya £4.5m, upande wa pili Bayern M
    unich kupitia kwa CEO wake Karl-Heinz Rummenigge imetangaza kukubali kumuuza kiungo wake Bastian Schweinsteiger kwenda Manchester United kwa ada ya £15m.

    Schweinsteiger,30 ambaye amedumu na Bayern Munich kwa miaka 17 na kushinda vikombe lukuki anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya mapema wiki ijayo kabla ya kusaini mkataba wa miaka mitatu wa kuwatumikia mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu ya England.

    Schweinsteiger anaiacha Bayern Munich akiwa ameichezea michezo 500 huku akifanikiwa kufunga jumla ya mabao 67.Pia ameisaidia Bayern kushinda jumla ya vikombe vinane vya Bundesliga pamoja na kombe moja la ligi ya mabingwa wa Ulaya mwaka 2013.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RASMI BAYERN MUNICH YAMUUZA SCHWEINSTEIGER KWENDA MANCHESTER UNITED Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top