728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, July 11, 2015

    CASILLAS AKUBALI KUSAINI MIAKA MIWILI PORTO,CIRO IMMOBILE AELEKEA RAMON SANCHEZ PIZJUAN,EL SHAARAWY NJIANI MONACO

    El Shaarawy:Monaco iko karibu kuipata saini ya mshambuliaji wa AC Milan El Shaarawy kwa ada ya €20m.El Shaarawy,22 atafanyiwa vipimo vya afya kesho jumapili.( Sky Sport Italia)

    Oblak:Manchester United itamsajili
    mlinda mlango wa Atletico Madrid Jan Oblak ikiwa mlinda mlango wake David De Gea atahamia Real Madrid.Ili kufanikisha mpango huo Manchester United italazimika kutoa ada ya €45m (£32m).(AS)

    Casillas:Iker Casillas amekubaliana na Real Madrid na sasa yuko tayari kujiunga na Porto FC.Casillas atasaini mkataba wa miaka miwili kuichezea miamba hiyo ya Ureno.(AS)

    Shaqiri:Xhedani Shaqiri amekubali kurejea tena Ujerumani lakini safari hii atajiunga na Schalke 04 baada kukataa kujiunga na Stoke City.(Sky Sport Italia)

    Delph:Manchester City inatarajia kufanya usajili wake wa kwanza kwa kumsajili kiungo wa Aston Villa Fabian Delph kwa ada ya uhamisho ya £8m.Delph ameachwa na kikosi cha Aston Villa ambacho kimesafiri kwenda Ireland kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu.Wakati Delph akitarajiwa kuondoka jana Aston Villa ilifanikiwa kumsajili kiungo wa Lille Idrissa Gueye kwa ada ya £8m.

    Immobile:Sevilla huenda ikamtangaza mshambuliaji Ciro Immobile 25 kuwa mchezaji wake mpya.Habari za kuaminika zinasema ofa ya €15m imekubali na Borussia Dortmund ambayo ndiyo inayommiliki nyota huyo toka Italia.(Marca)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CASILLAS AKUBALI KUSAINI MIAKA MIWILI PORTO,CIRO IMMOBILE AELEKEA RAMON SANCHEZ PIZJUAN,EL SHAARAWY NJIANI MONACO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top