Gervinho:Winga wa klabu ya As Roma Gervas Yao Quasi "Gervinho" ameachana na klabu yake hiyo na kutua katika klabu ya Al Jazira ya falme za kiarabu kwa
kitita cha €14m.Gervinho anahama Roma baada ya kudumu kwa misimu miwili pekee akitokea klabu ya Arsenal kwa kitita cha £8m.
Cech:Kocha Jose Mourinho amevionya vilabu vinavyomtaka mlinda mlango wake Peter Cech navyo vijiandae kupoteza wachezaji wao nyota kwani anahitaji kusajili mlinzi,kiungo na mshambuliaji.Vilabu vinavyomtaka Cech 33 ni Arsenal,Paris St-Germain na Besiktas.
Krychowiak:Klabu ya Arsenal imeripotiwa kufikiria kumsajili kiungo wa Sevilla Grzegorz Krychowiak badala ya Morgan Schneiderlin wa Southampton baada ya kuona vita ni kubwa katika mbio za kumnasa kiungo huyo toka Ufaransa.
Schneiderlin:Klabu ya Manchester United inaamini uhusiano mzuri uliopo kati yake na klabu ya Southampton utarahisisha upatikanaji wa kiungo mkabaji Morgan Schneiderlin,25.
Luiz:Mlinzi wa klabu ya Chelsea Felipe Luiz ameripotiwa kukataa ofa ya kujiunga na klabu ya Real Madrid na badala yake anataka kurejea katika klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha Jose Mourinho.
Varane:Klabu ya Manchester United imeulizia uwezekano wa kumsajili mlinzi wa klabu ya Real Madrid Raphael Varane mwenye mkataba mpaka 2020.
0 comments:
Post a Comment