UMOJA wa klabu zitakazoshiriki ligi daraja la kwanza (FDL) jana umefanikiwa kufanya kikao chake cha kwanza na cha kihistoria kujadili changamoto za ligi hiyo kuelekea msimu mpya wa 2015/2016.
Katibu mkuu na msemaji wa umoja huo,Masau Bwire amesema moja ya
changamoto waliyoieleza serikali, TFF na bodi ya ligi ni kukosekana kwa udhamini kunakowafanya wachezaji wa timu za FDL wafanye kazi kama wanajitolea.
"Kikao kimefanyika kwa ufanisi wa hali ya juu kwasababu hatukutarajia kama mahudhurio yangekuwa makubwa kiasi kile.Pia wageni tuliowaalika walifika, tumezungumza na kuwaambia nini tunataka kifanyike ili kuboresha ligi daraja la kwanza". Amesema Bwire na kuongeza:
"Tumezungumzia udhamini wa ligi daraja la kwanza, ligi haina udhamini, hali ambayo inavifanya vilabu vishindwe kumudu gharama, wachezaji wanacheza kama wanajitolea.
Yote haya tumeieleza serikali, TFF, Bodi ya ligi ili kuangalia namna ya kufanya kuboresha ligi hii".
Bwire pia ni msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting iliyoshuka daraja msimu wa 2014/2015 sambamba na maafande wa Polisi Morogoro.
0 comments:
Post a Comment