Habari na Paul Manjale
Nyota aliyekuwa na msimu mbaya katika klabu ya Manchester United Mcolombia Radamel Falcao jana usiku aliendelea kuwa yeye ni zaidi ya wengi wanavyodhani baada ya kuipatia ushindi wa goli 1-0 timu yake ya taifa dhidi ya Costa Rica katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Katika mchezo huo uliopigwa huko Buenos Aires,Argentina Falcao alionekana kuwa mchangamfu na msumbufu aliipatia goli hilo la pekee Colombia baada ya kuunganisha pasi safi ya winga Juan Cuadrado "Rasta"
Katika mchezo mwingine wa kirafiki uliopigwa huko San Juan Argentina ikiongozwa na nahodha wake wa muda Angel Di Maria ilijipatia ushindi wa goli 5-0 dhidi ya Bolivia.
Magoli ya Argentina yalifungwa na Di Maria (2) huku Sergio Aguero akifunga (3) hat-trik.
0 comments:
Post a Comment