Kocha, Piet De Mol raia wa Ubelgiji, ameendelea kuonyesha nia ya kutua kwenye klabu ya wakata miwa, Mtibwa Sugar, baada ya
viongozi wa timu hiyo kuthibitisha kuwa juzi Jumatatu alitembelea klabuni hapo.
viongozi wa timu hiyo kuthibitisha kuwa juzi Jumatatu alitembelea klabuni hapo.
Licha ya kutofanya mazungumzo yoyote ya kumpa mkataba, lakini uongozi huo umesema kuwa kocha huyo alifika Manungu Turiani kwa ajili ya kuangalia mandhari pamoja na kambi ya wachezaji kwa ujumla na namna wanavyoishi.
Msemaji wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru,alithibitisha ujio wa kocha huyo klabuni hapo ambapo alidai kuwa licha ya kuwatembelea lakini bado hawajafanya mazungumzo yoyote kuhusu usajili japokuwa nia ya kuzungumza naye ipo.
“Ni kweli jana (juzi) Jumatatu De Mol alifika hapa klabuni kwa ajili ya kucheki mandhari pamoja na kambi ya wachezaji wetu kwa ujumla.
“Licha ya kutua hapa,hatuna maana ya kwambatumeshamsajili,hapana,tunaomba tu mashabiki wetu wawe na subira, pindi tutakapomalizana naye tutawajuza kinachoendelea kwani nia tunayo juu yake,” alisema Kifaru.
0 comments:
Post a Comment