Aliyewahi kuwa straika wa Simba,Betram Mwombeki,ametangaza rasmi kuachana na soka baada ya kupatwa na majeraha ya muda mrefu.
Mwombeki ambaye alizitumikia Simba na JKT Ruvu kwa nyakati tofauti,kwa sasa yupo nyumbani kwao Mwanza akijishughulisha na
ufugaji na uvuvi kwa kile alichodai kuwa amerudia fani yake ya utotoni.
Mshambuliaji huyo alisema kwa sasa amelipa soka mgongo na kujikita katika ishu hizo.“Kwa sasa nimeachana na masuala ya soka na nimeamua kuirudia fani yangu ya zamani ambayo ni ufugaji na uvuvi na ninaifanyia huku nyumbani Mwanza.
“Sababu hasa iliyonifanya kuachana na soka ni kutokana na kuwa na majeraha ya muda mrefu kwani miguu ilikuwa inawaka moto chini ya unyayo nikaona siwezi tena kucheza mpira,” alisema Mwombeki.
"Unajua kila nilipokuwa najaribu kurejea uwanjani,miguu inauma sana kwenye unyayo kama vile inawaka moto.
"Nilijaribu kila mara kuhakikisha napona,matibabu yote nimepata lakini bado inashindikana.Nimeona niachane na soka hasa la Tanzania,"alisisitiza Mazungumzo yake yalionyesha ana hisia za ushirikina lakini hata hivyo hakutaka kufafanua zaidi.
Tokea alipojiunga na Ruvu,Mwombeki hakupata nafasi ya kuitumikia timu yake kutokana na kuwa na majeraha ya mara kwa mara hali iliyoonyesha kumkatisha tamaa.
0 comments:
Post a Comment