Habari na Paul Manjale
Siku za kiungo Abou Diaby ndani ya klabu ya Arsenal hatimaye zimefikia kikomo baada ya
klabu hiyo kumuengua katika kikosi chake cha msimu ujao.
Diaby ambaye alitua Arsenal mwaka 2006 akitokea klabu ya Auxier ya nyumbani kwao Ufaransa leo ametangazwa kutoongezewa mkataba mpya baada ya uliopo kuwa umefikia tamati.
Arsenal imefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na majerahi yake yasiyopona kwani mpaka sasa kiungo huyo mrefu ameumia zaidi ya mara 40.
Diaby anaondoka akiwa amefanikiwa kuifungia Arsenal jumla ya magoli 19 na kupika mengine 15
0 comments:
Post a Comment