728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, July 10, 2015

    USAJILI:MARCO VAN GINKEL ATUA STOKE CITY,LIVERPOOL YAMTAJA MBADALA WA STERLING,ARSENAL YAHAMIA KWA NDUGU WA ARDA TURAN

    Skrtel:Mlinzi wa Liverpool Martin Skrtel 30 amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu wa kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya Anfield mpaka mwaka 2019.

    Reus:Liverpool itaziba pengo la
    winga wake anayetaka kutimka klabuni hapo Raheem Sterling kwa kumsajili winga wa Dortmund Mjerumani Marco Reus (TalkSport )

    Austin:Crystal Palace inataka kuipa QPR kitita cha £6m pamoja na wachezaji wawili ili ipewe mshambuliaji Charlie Austin,25. (Guardian )

    Mitrovic:Newcastle huenda ndani ya masaa 24 ikatangaza kumsajili mshambuliaji mahiri wa Anderletch Aleksandar Mitrovic,20 kwa kitita cha £13m.

    Ginkel:Stoke City imemsajili kiungo wa Chelsea Mbelgiji Marco van Ginkel kwa uhamisho wa mkopo wa msimu mmoja.Usajili huo wa Ginkel,22 unatoa nafasi kwa Chelsea kumsajili mlinda mlango wa Stoke City Asmir Begovic kwa kitita cha £8m.

    Ogbonna:West ham imefanikiwa kumsajili mlinzi wa Juventus Angelo Ogbonna,27 kwa ada ya £8m.Ogbonna nyota wa zamani wa Torino amesaini mkataba wa miaka minne.

    Topal:Arsenal imeripotiwa kuitaka saini ya kiungo mkabaji wa Fenerbahce Mturuki Mehmet Topal,29 baada ya kutuma ofa ya €7m.Mbali ya Arsenal vilabu vingine vinavyomtaka nyota huyo ni Liverpool na Everton

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:MARCO VAN GINKEL ATUA STOKE CITY,LIVERPOOL YAMTAJA MBADALA WA STERLING,ARSENAL YAHAMIA KWA NDUGU WA ARDA TURAN Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top