728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, July 05, 2015

    NASRI:MIMI NIRUDI ARSENAL!?THUBUTU!

    Paris,Ufaransa.

    Kiungo wa klabu ya Manchester City Mfaransa Samir Nasri ameibuka na kupinga vikali habari zilizoenea kuwa ameomba kurejea katika klabu yake ya zamani ya Arsenal baada ya kuona mambo ni magumu pale Etihad.

    Nasri amechukua hatua hiyo baada ya mapema siku ya alhamisi chombo kimoja cha habari cha England kuripoti kuwa kiungo huyo alifanya mawasiliano na kocha wa Arsenal Arsene Wenger na kuomba arudi katika klabu hiyo aliyoikacha mwaka 2011.

    Nasri mwenye miaka 28 sasa jana jumamosi alitumia ukurasa wake wa twitter kukanusha habari hizo na kusisitiza kuwa hana mpango wa kurudi katika klabu hiyo ya London na kuongeza kuwa bado ana furaha katika klabu yake ya Manchester City.

    Ujumbe huo wa twitter ulisomeka hivi "Mimi kurudi Arsenal???Acheni habari zenu za kipuuzi!!

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NASRI:MIMI NIRUDI ARSENAL!?THUBUTU! Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top