Lagos,Nigeria.
Chama cha soka nchini Nigeria (NFF) kimemfuta kazi kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Steven Keshi.
Taarifa rasmi iliyotolewa mapema leo hii na NFF imesema chama hicho kimeamua kumfuta kazi Keshi kutokana na kushindwa kutimiza majukumu anayopewa na wakuu wake.
Hii ni mara ya pili kwa Steven Keshi kutupiwa virago na NFF kutokana na tuhumu mbalimbali lakini wadadisi wa mambo wanasema sababu nyingine iliyofanya kocha kuyo afutwe kazi ni baada ya hivi karibuni kutuma maombi ya kuifundisha timu ya taifa ya Ivory Coast.Kitendo ambacho kimewauzi maafisa wa NFF.
Wakati huo huo NFF imewachagua Salisu Yusuf na Shaibu Amodu kuwa makocha wa muda wa Super Eagle mpaka hapo kocha mpya atakapopatikana.
0 comments:
Post a Comment