728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, July 05, 2015

    MAN UNITED YACHEMSHA KWA TURAN YAHAMIA KWA BEGOVIC,ARSENAL YAMFUATA MTOTO WA KIARABU


    Begovic:Klabu ya Manchester United inajiandaa kuipiku klabu ya Chelsea kwa kumsajili mlinda mlango wa klabu ya Stoke City Asmir Begovic mwenye thamani ya £8m.(Daily Mail)

    Benteke:Usajili wa
    mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke kwenda Liverpool umeendelea kuchukua sura mpya baada miamba hiyo ya Anfield kutokuwa tayari kutoa kitita cha £32.5m ili kumsajili nyota huyo raia wa Ubelgiji huku nayo Aston Villa ikiwa haina mpango wa kushusha bei.(Daily Mail)

    De Bruyne:Manchester City imeripotiwa kupanga kubisha hodi katika klabu ya Wolfsburg na kitita cha £50m kwa ajili ya kumsajili kiungo Kevin de Bruyne.(Sunday Telegraph)

    Callejon:Atletico Madrid inataka kumsajili winga wa Napoli ambaye aliwahi pia kuichezea Real Madrid Jose Callejon kwa ajili ya kuziba nafasi ya Arda Turan anayetimka klabuni hapo.Habari za ndani zinasema tayari Atletico Madrid imeandaa kitita cha €12m ili kufanikisha mpango huo mapema.(Sport Italia)

    Turan:Klabu ya Manchester United imejitoa katika mbio za kumsajili kiungo wa Atletico Madrid Mturuki Arda Turan na badala yake itaelekeza nguvu zake katika kukamilisha usajili wa kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin.(Daily Mail)

    Darmian:Manchester United inataka kumsajili mlinzi wa kulia wa klabu ya Torino Matteo Darmian.Ili kufanikisha mpango huo Manchester United itapaswa kutoa kitita cha €20m.(Sky Sport Italia

    Alderweireld:Mmiliki wa Tottenham Daniel Levy amewasili katika jiji la Madrid kunako makao makuu ya klabu ya Atletico Madrid kwa ajili ya kukamilisha usajili wa mlinzi wa klabu hiyo Toby Alderweireld aliyefanya vizuri msimu uliopita akiwa na Southampton kwa mkopo.(Daily Mail)

    Rodriques:Liverpool huenda ikaendelea  kuongeza sura mpya katika kikosi chake baada ya kuripotiwa kuwa katika mpango wa kumsajili kinda wa Kibrazili Allan Rodrigues de Souza.Allan,18 ni mmoja kati ya nyota wanaofanya vizuri katika klabu ya Internacional.(Liverpool Echo)

    Austin:Newcastle United mapema wiki ijayo itatuma ofa rasmi ya £15m kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa QPR Charlie Austin.Wakati huo huo kocha Steve McClaren ana amini ukaribu uliopo kati yake na Austin utasaidia kufanikisha usajili.(Sunday Express)

    Pogba:Manchester City inataka kuweka rekodi ya usajili nchini England baada ya kuripotiwa kuwa tayari kumnunua kiungo wa Juventus Paul Pogba kwa ada ya €100m.Manchester City imetangaza ofa hiyo baada ya mapema wiki iliyopita Barcelona kutenga €80m kwa ajili ya kuipata saini ya kiungo huyo Mfaransa.(Sunday Mirror)

    Munir:Arsenal ipo katika mazungumzo na Barcelona kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo Munir El Haddadi mwenye umri wa miaka 19.(The Express)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAN UNITED YACHEMSHA KWA TURAN YAHAMIA KWA BEGOVIC,ARSENAL YAMFUATA MTOTO WA KIARABU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top