728x90 AdSpace

Sunday, July 05, 2015

MKWASA:STARS IMEPIGA HATUA JAPO KUNA MAKOSA KIDOGO

Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kilifanya vema na kufanya makosa kadhaa katika mechi dhidi ya Uganda kuwania kucheza michuano ya Chan.

Lakini akasisitiza kuwa ku
na mabadiliko makubwa ambayo yamejionyesha na yanaweza kuwa msaada baadaye katika kikosi hicho.

Stars ilitoka sare ya bao 1-1 na wenyeji wake Uganda katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Nakivubo, Kampala.

“Utaona kulikuwa na mabadiliko makubwa na tunaweza kuendelea kufanya mabadiliko zaidi kwa kuwa tumekuwa na muda mfupi sana.

“Matumaini yetu kama benchi la ufundi ni kubadilika zaidi kwa ajili ya mechi zijazo,” alisema Mkwasa.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MKWASA:STARS IMEPIGA HATUA JAPO KUNA MAKOSA KIDOGO Rating: 5 Reviewed By: Unknown