728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, July 05, 2015

    JENS LEHMANN AMPA DARASA MESUT OZIL

    Gwiji na mlinda mlango wa zamani wa klabu ya Arsenal Mjerumani Jens Lehmann amemtolea uvivu kiungo wa klabu yake hiyo ya zamani Mesut Ozil na kumtaka afanye makubwa msimu ujao
    ili kuthibitisha thamani yake.

    Akiongea na gazeti la The Sun la nchini England Lehmann amesema "Kila mtu anajua kuwa Ozil anaweza kuwa mchezaji mzuri lakini ili kuthibitisha hilo anapaswa kuonyesha kiwango kizuri kwenye kila mechi.

    "'"Huitaji kuwa mchezaji mzuri katika mechi ndogo na kisha kuwa hovyo katika mechi kubwa".

    Ozil,26 aliyetua Arsenal mwaka 2013 akitokea Real Madrid kwa kitita rekodi cha £42.5m amekuwa akisakamwa mara kwa mara na mashabiki pamoja na wachambuzi wa soka kutokana na kushindwa kuwika katika mechi kubwa.

    Hata hivyo Lehmann anaamini bado nyota huyo anaweza kuwa staa mkubwa klabuni hapo Siku za usoni ikiwa atajirekebisha na kuondoa udhaifu huo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: JENS LEHMANN AMPA DARASA MESUT OZIL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top