Klabu ya Arsenal imeanza kukumbwa na balaa la majeruhi hata kabla ligi haijaanza hii ni baada ya kiungo wake mkongwe Thomas Rosicky kuendelea kusumbuliwa na maumivu ya goti yatakayomuweka
nnje kwa muda wa wiki tano.
Rosicky,34 ambaye hakuwemo kwenye kikosi cha Arsenal kilichosafiri juzi jumapili kuelekea Singopore kushiriki michuano ya Backleys Asia Trophy alipata jeraha hilo mwezi uliopita wakati akiitumikia timu yake ya Czeck katika michuano ya kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Ulaya (Euro 2016).
Hapo mwanzo jeraha hilo halikudhaniwa kuwa lingekuwa kubwa lakini baada ya kufanyiwa vipimo zaidi imegundulika kuwa tatizo ni kubwa kuliko ilivyodhaniwa mwanzo hiyo kiungo huyo atakosa mechi za kwanza za ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu.
0 comments:
Post a Comment