728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 14, 2015

    KOCHA SIMBA ATAKA KIPA MPYA,WALIOPO MMHH!!

    Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr ameuambia uongozi wa Simba ufanye kila linalowezekana kusajili kipa mwingine.

    Kerr raia wa Uingereza amenusa mbele
    na kuona kipa aliyeiva katika kikosi chake ni Ivo Mapunda pekee.
    Hivyo lazima awe na kipa mwingine iwapo itatokea dharura.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amethibitisha kuwa ni kweli, Kerr anataka kipa.

    “Kweli na tumeanza kulifanyia kazi suala hilo. Tunaendelea kusaka kipa sehemu mbalimbali ili kutimiza hilo ombi la kocha.
    “Wakati wa michuano ya Kagame pia tutaendelea kutafuta kipa. Ni suala la kiufundi, hivyo linahitaji utulivu, kuangalia na kushariana,” alisema Hans Poppe.

    Kipa mwingine wa Simba ni Peter Manyika ambaye alipata nafasi ya kukitumikia kikosi hicho msimu uliopita.
    Pamoja na kujitahidi, Manyika alifanya makosa kadhaa makubwa yaliyoisababishia Simba matatizo, lakini Simba walionyesha uvumilivu wakiamini ndiyo anajifunza.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOCHA SIMBA ATAKA KIPA MPYA,WALIOPO MMHH!! Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top