Baada ya kufanya vibaya katika ligi ya EPL mambo ndani ya klabu ya Liverpool yameanza kupamba moto baada ya klabu hiyo kuamua kuwatupia virago makocha wake wawili wasaidizi Colin Pascoe na Mike Marsh hapo siku ya jana ijumaa.
Pascoe ambaye ni rafiki mkubwa wa kocha Brendan Rodgers tangu wakiwa wote Swansea City amesitishiwa mkataba wake ikiwa imebaki miezi 12 ufikie tamati.
Naye Mike Marsh ambaye ni kiungo wa zamani wa klabu hiyo yeye mkataba wake umefikia kikomo na uongozi ulio chini ya mwenyekitiTom Werner umegoma kumuongeza.
Wakati huo huo majina ya nyota wengine wa klabu hiyo Sami Hyypia,Bolo Zenden na Jammie Carragher yametajwa kuziba nafasi hizo nyeti kabisa katika soka.
0 comments:
Post a Comment