728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 06, 2015

    OZIL AWATOLEA UVIVU WAJERUMANI

    Habari na Paul Manjale

    Kiungo wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil ameeleza jinsi anavyochukizwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo ya Ulaya.

    Ozil ambaye mapema wiki hii amefanya mahojiano na gazeti la Bild la nchi humo amesema wazi wazi kukerwa na tabia ya vyombo vya habari vya Ujerumani kumuuita Mjerumani Mturuki.

    Ozil ambaye ana asili ya Uturuki amesema ™Nadhani watu wamesahau kuwa nimezaliwa Gelsenkirchen (Ujerumani) na kukulia Ujerumani.

    Najivunia kujua mengi kuhusu mambo mengi ya nchi hii kama nidhamu na mafunzo ya soka pia nimejifunza mengi kuhusu soka la Uturuki kupitia Television.

    Ozil ameongeza ™Napenda watu wanione kuwa mimi ni mjerumani kama walivyo wajerumani wengine.Kwanini hawamuiti Sami Khedira Mjerumani-Mtunisia au Lukas Podolski na Miroslav Klose “Wajerumani-Wapolandi."?Alihoji Ozil.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: OZIL AWATOLEA UVIVU WAJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top