Ljubljana,Slovenia.
Timu ya taifa ya England imeendelea kuisogelea tiketi ya michuano ijayo ya Euro 2016 baada ya usiku wa leo kuibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya timu ya taifa ya Slovenia huko Ljubljana.
Wenyeji Slovenia walipata magoli
yao kupitia kwa wachezaji wake Milivoje Novakovic na Nejc Pecnik huku England ikipata magoli yake kupitia kwa kiungo Jack Wilshere aliyefunga magoli 2 na Wayne Rooney aliyefunga goli 1.
Baada ya magoli hayo Wishere ambaye wakuwahi kufunga goli lolote katika michezo 27 anaingia katika orodha ndefu ya viungo wa England waliowahi kufunga magoli wakiwa na timu yao ya taifa.
Bobby Charlton magoli 49 akicheza kama kiungo,David Beckham magoli 14,Frank Lampard magoli 29 katika michezo106,Steven Gerrard magoli 21 katika michezo114.Jack Wilshere magoli 2,Andros Townsend magoli 2 na James Milner 1,David Platt magoli 27 kati ya mwaka 1989 na 1996,Bryan Robson magoli 26 katika kipindi cha miaka nane.
Kufuatia ushindi huo England imendelea kuongoza kundi E ikiwa na alama 18.
Matokeo mengine ya michezo mingine ya Euro.......
FT Ukraine 3-0Luxembourg
FT Belarus 0-1 Spain
FT Slovakia 2-1 FYR Macedonia
FT Estonia 2-0 San Marino
FT Slovenia 2-3 England
FT Lithuania 1-2 Switzerland
FT Liechtenstein 1-1 Moldova
FT Russia 0-1Austria
FT Sweden 3-1Montenegro
FT Belarus 0-1 Spain
FT Slovakia 2-1 FYR Macedonia
FT Estonia 2-0 San Marino
FT Slovenia 2-3 England
FT Lithuania 1-2 Switzerland
FT Liechtenstein 1-1 Moldova
FT Russia 0-1Austria
FT Sweden 3-1Montenegro
0 comments:
Post a Comment