Shirikisho la soka Tanzania (TFF) leo limeamua mchezaji Ramadhan Singano yuko huru na sasa anaweza kujiunga na klabu yoyote ile.
Taarifa kutoka kwenye kikao cha Sheria haki na hadhi za wachezaji kilichokaa leo zinasema Simba SC walishindwa kutekeleza baadhi ya vipengele vya mkataba hivyo wanapoteza haki ya kummiliki nyota huyo.
Moja kati ya vipengele hivyo ni Simba SC kushindwa kumpatia nyumba ya kuishi Singano kama ilivyoanishwa katika mkataba walioingia naye.
0 comments:
Post a Comment