Chelsea wako tayari kutoa kiticha cha m £11m kwa mwaka ili kuutumia uwanja wa Wembley Stadium kwa misimu mitatu wakati uwanja
wake wa Stamford Bridge ukifanyiwa upanuzi toka watazamaji 42,000 mpaka 60,000.
Gazeti la Times limeripoti Chelsea,ambao watahitaji uwanja wa muda msimu wa 2017-18 tayari wameifikisha ofa kwenye bodi ya usimamizi ya uwanja wa Wembley.
Mbali na Chelsea,klabu ya Tottenham nayo iko katika mbio za kutaka kuutumia uwanja huo na tayari imeandaa ofa ya £8m ili kutimiza lengo hilo na kupisha marekebisho yanayotakiwa kufanywa katika uwanja wake wa White hart Lane.
The Times limeendelea kutanabaisha kuwa licha ya ofa hizo kubwa lakini bado bodi ya usimamizi wa Wembley haijaamua iwapo itaupangisha uwanja huo ama la.
Ikiwa mpango huo utakwama Chelsea itahamia katika uwanja wa Twickenham ambao ni maarufu kwa mchezo wa Rugby.
0 comments:
Post a Comment