728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 07, 2015

    OSPINA NABAKI ARSENAL KUMUWEKA CECH BENCHI,FLAMINI AITIWA ULAJI UFARANSA,MAN UNITED MBIONI KUMNASA DANI ALVES WA ITALIA

    Ospina:Mlinda mlango wa Arsenal Mcolombia David Ospina 28 amesema licha ya klabu hiyo kumsajili mlinda mlango nguri Peter
    Cech hawezi kuondoka klabuni hapo na badala yake atafanya kila awezalo ili aendelee kuwa chaguo la kwanza.

    Akiongea na jarida moja la nyumbani kwako Colombia,Ospina amesema "Nimezoea kugombea namba.Katika vilabu vyote nilivyopita nimekuwa nikipambana na hali hii na kuishia.Unapokuwa klabu kubwa kama Arsenal tegemea nyota wapya kuongezwa kwa ajili ya kuimarisha kikosi.Siri ya kufanikiwa ni kumshawishi kocha kwa kufanya vizuri mazoezini.


    Darmian:Toka Italia taarifa zinasema klabu ya Manchester United iko katika hatua nzuri ya kumsajili mlinzi wa kulia wa klabu ya Torino Matteo Darmian baada ya klabu hiyo ya England kukubali kutoa ada ya uhamisho ya £12.7m (€18m).

    Darmian ambaye kiuchezaji anafananishwa na mlinzi wa Barcelona Dani Alves ni miongoni mwa nyota waliofanya vizuri sana msimu uliopita akiwa na kikosi cha Torino kilichovichachafya vilabu vikubwa vya Juventus,Ac Milan,Inter Milan na AS Roma.

    Ikiwa Manchester United itafanikiwa kumsajili nyota huyu basi itakuwa imelamba dume kwani licha ya kuwa Darmian ni mlinzi wa kulia lakini pia ni mzuri katika nafasi ya ulinzi wa kati kutokana na uwezo wa kumudu mipira ya juu.

    Flamini:Klabu ya Bastia ya nchini Ufaransa huenda ikamsajili kiungo wa Arsenal Mfaransa Mathieu Flamini,31 baada ya klabu hiyo kuripotiwa kufungua mazungumzo rasmi ya kutaka kumsajili nyota huyo aliyewahi kukipiga pia na klabu ya AC Milan.lamini:Klabu ya Bastia ya nchini Ufaransa huenda ikamsajili kiungo wa Arsenal Mfaransa Mathieu Flamini,31 baada ya klabu hiyo kuripotiwa kufungua mazungumzo rasmi ya kutaka kumsajili nyota huyo aliyewahi kukipiga pia na klabu ya AC Milan


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: OSPINA NABAKI ARSENAL KUMUWEKA CECH BENCHI,FLAMINI AITIWA ULAJI UFARANSA,MAN UNITED MBIONI KUMNASA DANI ALVES WA ITALIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top