Mashabiki wa Liverpool wamepinga mpango wa klabu yao kutaka kuzitumia pesa za mauzo ya winga Raheem Sterling kwenda Manchester City (£49m) kumnunua mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke na badala yake wametaka pesa hizo zitumike kumnunua mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette.
Mashabiki hao licha ya kusema dau la Benteke ni kubwa pia wanaona kuwa mshambuliaji huyo haendani na mchezo wa kasi wa klabu hiyo.
Wakati huo huo polisi wa jiji la Liverpool wameanza msako wa kuwasaka mashabiki ambao wanadhaniwa kuwa wa Liverpool kutokana na kumtishia maisha winga Raheem Sterling mara baada ya kupata habari kuwa nyota huyo ataihama klabu hiyo na kujiunga na Manchester City kwa dau la £49m.
Mashabiki hao waliotumia mtandao wa twitter licha ya kumtukana,kumtolea maneno ya kibaguzi Raheem Sterling pia wametishia kumteka nyara mtoto wake wa kike aitwaye Melody Rose (3).
0 comments:
Post a Comment