Kikosi cha Stand United cha mjini Shinyanga kimeingia kwenye listi ya timu tajiri zaidi zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Stand inaingia kwenye listi hiyo na kuungana na timu nyingine za Yanga, Simba na Azam FC ambazo zina fedha nyingi na zinaweza kusajili kwa mamilioni ya fedha.
Kuingia huko ni baada ya kupata mkataba mnono wa miaka miwili na kampuni ya uchimbaji madi
ni ya Acacia ambao thamani yake ni bilioni 2.4.
Sasa ndiyo unakuwa mkataba mkubwa zaidi ukilinganishwa na ule wa Yanga na Simba kwa TBL ambazo zimekuwa zikiingiza hadi Sh milioni 320 kwa mwaka, ni mkataba wa miaka mitatu.
0 comments:
Post a Comment