728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, July 09, 2015

    ARTURO VIDAL ANUSURIKA KWENDA JELA, APEWA KAZI YA KUWAHUTUBIA WAFUNGWA


    Kabla ya hapo, Vidal anayekipiga Juventus ya Italia pia aliomba radhi kutokana na kuwadhalilisha askari polisi waliomkamata.Nyota wa Chile, Arturo Vidal amenusurika kwenda jela baada ya kupatikana na hatia ya kuendesha gari akiwa amelewa. Lakini mahakama ya San Bernardo
    karibu na jiji la Santiago, Chile ikapunguza makali ya adhabu hiyo.

    Alisababisha ajali hiyo siku kadhaa kabla ya michuano ya Copa America akiwa na gari lake la kifahari aina ya Ferrari.

    Vidal aliyeiongoza Chile kubeba ubingwa wa Copa America, amepunguziwa adhabu na sasa ametakiwa kulipa hasara alizowasababishia madereva wa magari mengine aliyoyagonga.

    Baada ya hapo, amepewa adhabu nyingine ya kwenda kutoa hutoba ya onyo na kuwapa matumaini wafungwa walio gerezani.

    Pia ameahidi kununua vifaa mbalimbali vya michezo kwa watoto na jamii.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARTURO VIDAL ANUSURIKA KWENDA JELA, APEWA KAZI YA KUWAHUTUBIA WAFUNGWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top