Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ameonyesha kuumizwa na maneno yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Wakati akilifunga Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Kikwete aliamua kuwa wazi na kusema aliamua kuacha kwenda uwanjani kuiunga mkono Taifa Stars kutokana na kupoteza michezo mfululizo.
Kikwete alisema mara kadhaa alipokuwa akienda uwanjani, Stars ilikuwa ikipoteza hadi kufikia kuona watu wanaweza kuona yeye ana bahati mbaya ndiyo maana timu inafungwa kila mara.
Hali hiyo ilimfanya Mkwasa ajitokeze na katika maneno yake alisisitiza kuwa ni wakati mwafaka kwa Kikwete kurudisha imani yake kwa Stars kwa kuwa imebadilika.
0 comments:
Post a Comment