728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, July 15, 2015

    KIUNGO STAND UNITED APATA TIMU UJERUMANI, ASAINI MIAKA MIWILI

    Mtanzania Charles Misheto amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu ya Rabestein FC ya nchini Ujerumani.

    Rabestein FC inashiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ujerumani na Mishetto aliyekuwa kiungo wa zamani wa Stand United ya Shinyanga, tayari amesaini makataba huo.

    Akizungumza kutoka Ujerumani, Mishetto amefanikiwa kusaini mkataba na timu hiyo.

    “Ingawa awali nilikuwa nafanya majaribio na timu nyingine, lakini sasa nimefanikiwa kusajiliwa na timu nyingine ya daraja la nne ambayo ilianza kuniwania,” alisema.

    “Nilikuja hapa, nikafanya nao mazoezi kwa siku mbili, baada ya hapo wamekubaliana na uwezo wangu, tumesaini mkataba.”

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KIUNGO STAND UNITED APATA TIMU UJERUMANI, ASAINI MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top