728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, July 15, 2015

    TFF YATEUA KAMATI YA USHAURI YA LIGI KUU

    Rais wa Shirikiso la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Jamal Malinzi ameteua Kamati ya ushauri ya Ligi Kuu (VPL) na ligi Daraja la Kwanza (FDL) nchini.

    Mwenyekiti wa Kamati hiyo ni Alhaj Ahmed Mgoyi na katibu wa Kamati ni mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi nchini (TPLB) na wajumbe wengine saba.

    1. Alhaji Ahmed Idd Mgoyi (Mwenyekiti)
    2. Boniface Wambura (Katibu)
    3. Kennedy Mwaisabula- Mjumbe
    4. Idd Mshangama- Mjumbe
    5. Amiri Mhando- Mjumbe
    6. Grace Hoka- Mjumbe
    7. Ibrahim Kaude (Vodacom)- Mjumbe
    8. Baruan Muhuza (Azam Media)- Mjumbe
    9. Peter Simon- Mjumbe

    Kazi za kamati hiyo zitakua ni:
    (i) Kufuatilia mwenendo wa Ligi
    (ii) Kuishauri Bodi/TFF namna ya kuboresha Ligi
    (iii) Masoko
    (iv) Leseni za Vilabu (Club Licensing)
    (v) Mipango ya Maendeleo ya Vilabu
    (vi) Viwanja vya mazoezi
    (vii) Utoaji wa tuzo za ligi mbalimbali
    (viii) Kutengeneza vigezo (criteria) vya washindi wa tuzo


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TFF YATEUA KAMATI YA USHAURI YA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top