728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, July 15, 2015

    KIUNGO LIVERPOOL AMKATAA RAHEEM STERLING

    Kiungo wa Liverpool Mbrazil Lukas Leiva amesema kuondoka kwa winga Raheem Sterling hakutaiumiza klabu hiyo kama ilivyokuwa kwa mshambuliaji Louis Suarez aliyetimikia Barcelona msimu
    mmoja uliopita.

    Akiongea kutoka Thailand ilikoweka kambi klabu hiyo Lukas amesema "Nadhani haitakuwa haki kumfananisha Sterling na Suarez.Ni mdogo bado.Ndiyo kwanza ana miaka 20.Bado ana mengi ya kujifunza.

    Nakiri Sterling alikuwa ni mchezaji muhimu sana misimu miwili iliyopita lakini kuondoka kwa Suarez ilikuwa ni pigo kubwa sana kwetu.

    Suarez ni mmoja kati ya washambuliaji bora sana kwa sasa na Sterling ni mmoja kati ya makinda bora sana kwa sasa.Hivyo ukitazama utaona kuna tofauti kubwa kati yao".



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KIUNGO LIVERPOOL AMKATAA RAHEEM STERLING Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top