728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, July 15, 2015

    MICHU AIKACHA SWANSEA,PEDRO KUSAINI CHELSEA WIKI IJAYO,WAKALA ASEMA LEWANDOWSKI ANAHAMISHIKA KWA BEI HII

    Campbell:Rasmi Klabu ya Real Sociedad inayonolewa na kocha David Moyes imetuma ofa ya £6m kwa klabu ya Arsenal kwa ajili ya kuinasa saini ya kinda Joel Campbell,23.(Daily Mirror)

    Pedro:Chelsea imeripotiwa kufikia dau la £22m ambalo ni bei iliyopangwa na Barcelona kwa nyota wake Pedro.Habari kutoka Hispania zinasema wiki ijayo dili la uhamisho wa nyota huyo huenda likakamilika.(Daily Star)

    Sanogo:Mshambuliaji wa Arsenal Yaya Sanogo kesho alhamisi anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wa kuichezea klabu ya Ajax kwa mkopo wa msimu mmoja.(De Telegraaph)

    Dos Santon:LA Galaxy imefanikiwa kumsajili kwa mkataba wa miaka minne na nusu nyota wa zamani wa vilabu vya Villareal,Barcelona na Tottenham Giovani dos Santos.

    El Ouriachi:Stoke City imemsajili kinda wa Barcelona Moha El Ouriachi. El Ouriachi 19 ametua Stoke City baada ya kukataa mkataba mpya aliopewa na Barcelona.Mpaka sasa Stoke City ina wachezaji watatu toka Barcelona ambao ni Bojan,Marc Muniesa na El Ouriachi.

    Lewandowski:Wakala wa mshambuliaji Robert Lewandowski aitwaye Cezary Kucharski amesema mteja wake anaweza kuihama Bayern Munich ikiwa vilabu vya Arsenal na Manchester United vitatoa kitita cha £35m.

    Michu:Mshambuliaji wa Swansea City Michu,29 hatoichezea tena klabu hiyo na sasa anajiandaa kurudi nyumbani kwao Hispania.Kocha wa Swansea Garry Monk amesema Michu ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara tayari ameshaitaarifu klabu hiyo juu ya mpango huo kinachosubiriwa na kauli ya mwenyekiti wa klabu hiyo.







    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MICHU AIKACHA SWANSEA,PEDRO KUSAINI CHELSEA WIKI IJAYO,WAKALA ASEMA LEWANDOWSKI ANAHAMISHIKA KWA BEI HII Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top