Kiungo wa zamani wa Arsenal ambaye kwa sasa anachezea UFA ya Urisi Emmanuel Frimpong huenda akafungiwa kucheza kwa kipindi kirefu baada ya kuwatukana mashabiki wa Sparkat Moscow baada ya kufanyiwa vitendo vya kibaguzi jana ijumaa katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya Urusi.
KADI NYEKUNDU
Frimpong,23 aliteleza na kupoteza mpira kisha akamchezea rafu mbaya mchezaji wa Spartak.Kufuatia tukio hilo mashabiki wa Spartak Moscow wakaanza kumzomea na kumuita nyani mchezaji huyo mzaliwa wa Ghana.
AKAJIBU MAPIGO
Frimpong alijibu mapigo kwa kuwaonyesha kidole cha kati ambayo ni ishara ya matusi kitendo ambacho kilimfanya alimwe kadi nyekundu dakika ya 32 ya mchezo.Michezo huo uliisha kwa matokeo ya sare ya 2-2.
FRIMPONG ANASEMAJE
Frimpong akitumia mtandao wake wa twitter amesema
"Nimebaguliwa katika mchezo niupendao.Nakwenda kufungiwa baada ya kubaguliwa kisa mimi ni mtu mweusi.Ni aibu sana kwa nchi hii ambayo mwaka 2018 ataandaa fainali za kombe la dunia.
JE,HALI IKOJE URUSI?
Tangu mwaka 2013 wachezaji watatu weusi wameshafungiwa kati ya michezo miwili mpaka minne baada ya kuwatukana mashabiki waliowafanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi.
0 comments:
Post a Comment