Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema kikosi chake kimepoteza mchezo dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kutokana na mambo mengi ambayo wanaweza kujifunza.
Lakini akasisitiza, kuna kila sababu ya kuangalia mechi zinazokuja kwa lengo la kufanya vizuri.
“Utaona kuna mambo tumekosea, kuna mambo hatukuwa makini. Wakati mwingine hata mwamuzi hakuwa makini pia.
“Lakini inabaki hivi; makosa hayo yawe kama fundisho kwetu na tuangalie kwa ajili ya mechi ya pili.
“Tunatakiwa kushinda mechi zote zilizobaki kwenye kundi ili kusonga mbele,” alisema Pluijm.
Yanga imeanza michuano ya Kombe la Cecafa kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
Hata hivyo, Yanga itajilaumu yenye kutokana na kadi nyekundu ya Ronald Ngoma mapema katika kipindi cha kwanza.
Lakini ikapata penalti katika kipindi cha pili, bado ikashindwa kuitumia baada ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’
0 comments:
Post a Comment