728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 14, 2015

    VILABU VYA UTURUKI VYATAKA KUENDELEA KUIGEZA MAN UNITED SHAMBA LA BIBI,MAN CITY YATAJA DAU LA DZEKO,DI MARIA AKUBALIANA NA PSG

    Raheem Sterling huenda muda wowote kuanzia sasa akatangazwa kuwa mchezaji mpya wa Manchester City baada ya nyota huyo kuripotiwa kuanza vipimo vya afya mapema leo asubuhi.Ikiwa Sterling
    atafuzu vipimo hivyo atasaini mkataba ambao utamuwezesha kuvuna £180,000 kwa wiki.

    Sanogo:Mshambuliaji Yaya Sanogo huenda akatimka Arsenal na kujiunga na Ajax kwa uhamisho wa mkopo wa msimu mmoja.Taarifa za kuaminika zinadai vilabu hivyo viwili vimeshafikia makubaliano kilichobaki ni kumalizia masuala madogo madogo.

    De Bruyne:Baada ya kuwa mbioni kumnasa Raheem Sterling Manchester City imeendelea kuonyesha jeuri ya pesa baada ya kuripotiwa kuandaa kitita cha £35m (€50m) ili kumsajili kiungo nyota wa Wolfsburg Kevin De Bruyne.(Daily Express)

    Di Maria:Winga Angel Di Maria huenda akaihama klabu yake ya Manchester United baada ya taarifa kudai kuwa nyota huyo toka Argentina amekubaliana maslahi binafsi na klabu ya PSG yenye makao yake katika dimba la Parc des Princes.(Le Parisien)

    Dzeko:Manchester City imeiambia klabu ya Roma kuwa itakuwa tayari kumuuza mshambuliaji wake Edin Dzeko ikiwa kitita cha £20m (€28m) kitawekwa mezani.(TalkSpot)

    Hernandez:Javier Hernandez huenda akaihama Manchester United  na kutua Besiktas ya Uturuki.Beskitas imepania kumsajili nyota huyo mzaliwa wa Mexico na tayari imeshaandaa kitita cha €6m ili kumtwaa nyota huyo mwenye umri wa miaka 27.(Milliyet)

    Ghoulam:Arsenal imepeleka ofa ya £10m katika klabu ya Napoli kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa kushoto Mualgeria Faouzi Ghoulam,24.Ujio wa Ghoulam Arsenal utafungua milango kwa mlinzi Nacho Monreal kutimkia Atletico Bilbao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VILABU VYA UTURUKI VYATAKA KUENDELEA KUIGEZA MAN UNITED SHAMBA LA BIBI,MAN CITY YATAJA DAU LA DZEKO,DI MARIA AKUBALIANA NA PSG Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top