728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, July 09, 2015

    VALDIVIA APATA ULAJI UARABUNI,DI MARIA KUTUA PSG KWA €60M,MFUPA WAMCHELEWESHA SONG KUTUA WESTHAM


    Valdivia:Klabu ya Al Wahda imemsajili kiungo wa Chile Jorge Valdivia kwa mkataba wa miaka miwili.Valdivia, 31,ambaye kwa sasa yuko mwishoni kumaliza mkataba ka
    tika klabu ya Palmeiras ya Brazil amesaini mkataba wenye thamani ya  €2.5m (Dh10.13m)

    Carvalho:Liverpool huenda ikapata urahisi katika kuinasa saini ya kiungo wa 
    Real Madrid Asier Illarramendi 25 baada ya miamba hiyo ya Hispania kutangaza kumuuza ili kupata pesa za kumnunua kiungo wa Sporting Lisbon’s William Carvalho,23.(Express)

    Ogbonna:Ndani ya saa 48 zijazo klabu ya Westham itatangaza kumsajili mlinzi Angelo Ogbonna toka klabu ya Juventus.Ogbonna 27 yuko London akifanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho huo wenye thamani ya £8.5m.(Sky Sports)

    Song:Mpango wa klabu ya West Ham kumsajili kiungo wa Barcelona Mcameroun Alex Song umeingia dosari baada ya nyota huyo kubainika kuwa na kipande cha mfupa kinachoelea ndani ya mguu wake ikihofiwa kuwa mmoja kati ya mifupa ya mguu umevunjika.Kutokana na hali hiyo Song atafanyiwa upasuaji na kulazimika kuwa nnje ya dimba kwa muda miezi mitatu.(Daily Mail)

    Gaitan:Manchester United iko tayari kutoa pesa pamoja na mchezaji wake mmoja kati ya  Rafael au Javier Hernandez "Chicharito" kwa ajili ya kuinasa saini ya winga wa Benfika Nico Gaitan.(A Bola)

    Persie:Mshambuliaji Robin van Persie,31 ameanza hatua ya kwanza ya vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki.Habari za kuaminika zinasema matabibu wa Fenerbhace wako jijini Manchester wakimfanyia vipimo vya awali nyota huyo kabla ya kumalizia vipimo vingine Uturuki.Ikiwa mpango huo utaenda vizuri Robin Van Persie atasaini mkataba wa miaka minne wakati Manchester United ikitia kibindoni kitita cha £12m.(Sky Sport)

    Jovetic:Mshambuliaji wa Manchester City Stevan Jovetic 25 yuko katika hatua za mwisho hukamia Inter Milan kwa mkopo wa msimu mmoja wenye thamani ya €3m kabla ya kubaki moja kwa moja mwisho wa msimu kwa kitita cha €18.(Tuttosport)

    Di Maria:Kutoka Ufaransa habari zinasema winga wa Manchester United Angel Di Maria,27 atajiunga na klabu ya PSG kwa mkataba wa miaka minne wenye thamani ya  €60m.( Le Parisien)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VALDIVIA APATA ULAJI UARABUNI,DI MARIA KUTUA PSG KWA €60M,MFUPA WAMCHELEWESHA SONG KUTUA WESTHAM Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top