728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, July 15, 2015

    REAL MADRID NDIYO KLABU TAJIRI ZAIDI DUNIANI

    Real Madrid ndio timu tajiri zaidi kwa mwaka wa tatu mfululizo kulingana na jarida la biashara la Forbes.

    Kilabu hiyo ya Uhispania ina thamani ya pauni bilioni 2.08 huku timu ya soka ya Marekani Dallas Cowboys na ile ya New York Yankees zikichukua nafasi ya pili kwa pamoja na thamani ya pauni bilioni 2.04.

    Mahasimu wakubwa wa Real Madrid Barcelona wanachukua nafasi ya nne wakiwa na thamani ya pauni bilioni 2.02.

    Kilabu ya Manchester United iko katika nafasi ya tano kutoka nafasi ya tatu mwaka uliopita.

    Nafasi nyengine zilizosalia katika kumi bora zinachukuliwa na timu za michezo nchini Marekani.
    Timu nyengine za ligi ya Uingereza ni Mancity iliopo katika nafasi ya 29 ikiwa na thamani ya pauni milioni 890,Chelsea ikiwa na thamani ya pauni milioni 877 inachukua nafasi ya 31 na Arsenal yenye thamani ya pauni milioni 839 ikiwa katika nafasi ya 36.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: REAL MADRID NDIYO KLABU TAJIRI ZAIDI DUNIANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top